Rabu, 19 Juni 2013
HIZI NDIZO SABABU ZINAZOPELEKEA MWANAMKE KUSALITI NDOA YAKE
Kuna aina ya ujinga ambayo inaweza kuwepo kwenye vichwa vya baadhi ya wanaume kwamba wanawake ni chombo cha burudani.
Kwamba makutano ya kitandani ni pale mwanaume anapoamua na suala la mwanamke kufurahia tendo na kuridhika siyo la lazima. Hili ni kosa la kiwango cha juu sana.
Huwezi kuwalaumu vijana wa zama hizi kwa sababu ni utaratibu wa kizamani sana. Mama ndiye mwenye wajibu wa kuhakikisha familia inapata riziki. Aende shamba kulima, arudi nyumbani na mavuno, apike, akachote maji. Wakati baba akiamka anakwenda vijiweni kupiga soga na kuhudhuria vilabu vya pombe.
Baba huyohuyo mvivu asiyependa kazi, akirudi nyumbani bila kuzingatia utayari wa mwanamke wake, hulazimisha mapenzi. Hapo suala la mwanamke kuhitaji penzi halipo, vilevile mwanaume anapokuwa ameshakamilisha haja zake, hujiweka pembeni pasipo kujishughulisha kujua kama mwenzi wake ameridhika au kinyume chake.
Kuna watu huendeleza utaratibu huo, wanakosea sana. Mwanamke huhitaji mwanaume ambaye anamjali, anayejishughulisha katika kuziweka sawa hisia zake. Kama hutalijua hilo na kulifanyia kazi, utajikuta unasalitiwa wakati kila kitu kipo ndani ya uwezo wako.
Huwa inatokea hivi; Wewe unaendekeza ubinafsi kwenye mapenzi, unamfanya mwenzi wako kuwa na mawazo, kwani humfanyi akajione yupo kwenye kilele cha raha za mapenzi. Unampa unyonge na zaidi, anahisi umrundikia makwazo kichwani. Matokeo yake anakuwa hakuoni kama ni rafiki.
Katika mizunguko yake, anakutana na mwanaume ambaye anapozungumza naye, anamfanya atabasamu. Huyo jamaa anafanikiwa kumfanya acheke, kwa hiyo wanazungumza vizuri na wanaelewana kweli. Wewe ukirudi nyumbani huna habari na furaha yake, naye anajiweka mbali.
Uponaye nyumbani, wewe ukiwa chumbani yeye anakwenda sebuleni. Ikiwa upo sebuleni, anakupisha na kwenda kuketi chumbani. Huko anatumia muda wake kufurahi kwa ‘kuchati’ na mwanaume anayemfanya atabasamu, anayeweza kumchekesha. Anajiona mwenye amani sana anapowasiliana naye.
Matokeo yake sasa, anakuwa anafurahia wewe ukiwa haupo ili apate nafasi ya kufurahi na jamaa anayejua namna ya kucheza na hisia zake. Siku akikutana naye kitandani, kwa vile hisia zake zinakuwa katika hali muafaka, kwa hiyo anafurahia tendo na juu ya yote anafika kileleni, kwa hiyo anamuona mwanaume huyo ni wa kipekee. Yaani anampa sifa za juu sana.
Mapenzi ni hisia, weka mbali ulimbukeni kwamba utamfanya mwenzi wako afurahie tendo kwa namna utakavyokuwa unapanda na kushuka kwa kasi bila kuchoka. Uwe unaweza kugusa kila kona ya kuta zake kwa ufundi wa hali ya juu lakini yote hayo ni kazi bure kama hisia za mwanamke hazipo tayari.
Kujifanya hodari wa kutuama kifuani kwa muda mrefu ukidhani atakuona kijogoo kwamba unachelewa kufika mwisho, unajidanganya. Zaidi atakuona msumbufu usiyejua mapenzi. Change ni wewe ! hamka ewe mume bora upiganie ndoa yako!
Langganan:
Posting Komentar (Atom)
Tidak ada komentar:
Posting Komentar