YAFUATAYO NI MUHIMU KUZINGATIA UKIWA UNAENDA HONEYMOON.
Ni watu wachache wanaopata ushauri wa nini chakuandaa kwa ajili ya kwenda navyo kwenye fungate. Watu huwa busy na harusi, nani atavaa nini nk na kuwaachia maharusi peke yao jukumu zima la maandalizi ya fungate. Ndiyo, jukumu la kuandaa fungate ni la maharusi, ila sababu wote ni wageni katika suala hili ni lazima wapate ushauri wa nini cha kuandaana nini cha kubeba ili wasije kupungukiwa na kitu au kubeba vitu visivyo na ulazima. Hapa nimeandaa listi ya vitu ambavyo unapaswa kuwanavyo kwa ajili ya fungate, unaweza kuprint na kutick pale unapokuwa tayari kwenda honeymoon.
Vitambulisho na dokumenti muhimu
- Passport na IDs
- Leseni ya udereva
- Kadi za ATM
- Uthibitisho wa bookings za hoteli n.k
- Tikets
- Notebook yenye namba muhimu
- Dawa za kupunguza maumivu
- Dawa za kuzuia kuharisha
- Dettol
- Gozi na pamba
- Dawa zozote unazozitumia
- Dawa ya mswaki na mswaki
- Sanitary pads
- Vipodozi unavyotumia
- Pafyumu na deodorant
- Tissue papers
- Chanuo na kitana
- Nail clipper
- Wet wipes
- Sabuni ya kuogea na dodoki
- Losheni na mafuta
- Vipanio vya nywele
- Taulo
- Sandals
- Intimacy jelly
- Pamba za masikioni
- Nguo za kutosha kulingana na hali ya hewa unakoelekea na muda utakaokuwa huko. usibebe nguo za kiofisi (formal), chukua nguo za kukufanya uwe confortable (casual).
- Nguo za ndani za kutosha (wekeza kwenye nguo nzuri za kuvutia).
- Viatu vyepesi vya kuvaa
- Nguo za kuogelea (kama mtapendelea)
- Doti ya kanga / kitenge
- Shuka
- Kamera na betri / charger
- Simu za mkononi na charger (msiwashe simu hadi siku ya kuondoka)
- Sindano na uzi wa kushonea
- Mkasi mdogo
- Handbag
Tidak ada komentar:
Posting Komentar