Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu Wema Sepetu amepata shavu la nguvu baada ya kuingia mkataba na kampuni nywele, Darling Hair Tanzania kuwa msemaji na muuza sura wao.
Kwa mujibu wa fashion designer na meneja wa Wema, Martin Kadinda, mkataba huo unamfanya wema awe staa anayeongoza kwa kulipwa fedha nyingi kuliko wote Tanzania.
“#SheIsOfficial #MostExpensive Celeb in Tz #Thank DarlingHairTz #Ninachakujivunia kwa muda niliofanya kazi na wewe @wemasepetu.” Martin Kadinda ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Hakusema mkataba huo ni wa kiasi gani.
Mkataba huo unamfanya Wema ahusike kwenye upande wa promotion; yaani kuwa msemaji na sura ya Darling Hair Tanzania. So far mafaniko yameanza sababu websites kibao, ikiwemo hii ya Maraha Laivu, zimeanza kuandika na kuipatia kampuni hiyo publicity ya bure.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar